Ibada ya Ndoa

Angalizo: Kwenye hii Dunia ya Kibepari na Ndoa kwa Watu waliobalehe miaka mingi iliyopita – Basi kwa dharula sio lazima wanandoa kuishi katika Nyumba/Chumba Kimoja – Jambo la Kizingatia tu ni kuwa Mwenyezi Mungu ameweka laana nyingi kwa Wazinifu.

Ndoa ni Halali kwa Waliobalehe na wa jinsia Tofauti. Lazima wasiwe Maharimu na isihusishe Mwanamke aliyeolewa.

Kwetu ndoa yaweza kuwa ya Mke mmoja hadi Saba katika kipindi cha Uhai wangu na Mmoja au Wawili baada ya Kifo/kutoweka kwangu na kwa sababu binafsi inaweza husisha hadi wake wanne.

Anayefungisha ndoa lazima awe Mwanandoa Mwanaume kwa aliye wa Imani yetu au aliyehamia kwenye Imani yetu.

Lazima kila ndoa ilipiwe gharama sawa na bei ya nusu gramu ya dhahabu kwa wale wenye pato Zaidi ya gramu tatu za dhahabu kwa Mwaka kwa taasisi au Familia ya Zumbe10D na sio kwa watoto mnaopanga nyinyi hata kama wanadamu ya Masihi Ten’dii. Na kama hukuweza kabla ya ndoa linakuwa deni la kulipwa upesi mambo yakitengemaa kwa awamu tatu au chini ya hapo.

Ndoa nilazima ihudhuriwe na watu Zaidi ya 10 wakiwemo Mashahidi waadilifu wawili wa bibi Harusi na wawili wa Bwana Harusi

Katika Ibada ya Ndoa Wanandoa watatarajiwa kukubali kuoana bila Mashinikizo labda kwa kujipendekeza kwa hiari yao katika kusaka Baraka za Wazazi wema au Watakatifu wengine wakiwa wanatambua kuwa hilo sasa ni jukumu la Maisha yote.

Ataulizwa kwanza Mwanaume Kisha Mwanamke Kama amekubali kuoana, wote wakijibu ndio basi kwa Idhini ya Mungu Mwenye enzi na Baraka na Karama za Masihi Ahmad (Zumbe10D) utawabariki iwe ndoa Takatifu

Baada ya Baraka ya Ndoa Wanandoa watageukia Mbele, mume akiwa Kulia kwa Mkewe, Watasujudu kwa kumkusudia Mungu mwenye enzi na Kumshukuru kwa kusema “Shukrani zote unastahili wewe Mwenyezi Mungu naomba utulinde na kutupa heri nyingi”

Kisha watasimama, Watainama kwa kumkusudia Masihi Ahmad (Zumbe10D) na kusema “Familia yetu ni Watiifu kwa Kusudi na Taifa lako, Mungu mwenye enzi Akulinde wewe, Familia ya Kifalme na Familia zetu”

Kisha watasimama wima, Watainama tena kuwakusudia Wazazi na kusema “Tunashukuru kwa kila kitu na huku sio kutengana bali kukua, Tunaomba Baraka zenu katika maisha yetu mapya” na

Mwisho Watageukiana na kurudi nyuma hatua moja, Mwanamke atapiga Magoti na Mwanaume atasoma dua kumuomba “Ewe Mwenyezi Mungu nibariki kwa heri zote za ndoa na nilinde na shari zake, iwe heri na Wema mwanzo hadi mwisho.”

Na mwanamke naye atafanya hivyo hivyo akiwa bado amepiga Magoti na hapo Ibada ya kufungisha ndoa itakuwa imekwisha.

Itatolewa hotuba fupi na nasaha kutoka kwa Mtakatifu au Aliyetangulia katika ndoa, mwenye Imani na Hekima.

Itafuatiwa na Sherehe kama ilivyopangwa kwa mujibu wa uwezo na wasaa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *