
Pichani ni Masihi Ahmad na Alama zake za Msingi. Picha hiyo imesanifiwa kwa Akili Sanifiwa
Mimi Ahmad Ten’dii ni Nabii, Mjumbe (Mtume) na Masihi (Mfalme) kutoka kwa Mungu Mwenye Enzi. Hii inamaanisha kwamba nafahamu siri zilizofichikana kwa Maksudi yake Mwenyezi Mungu yaani mambo ya ghaibu. Na hiyo ndio maana ya Nabii. Mjumbe wa Mungu hutumwa kwa Jamii au Zama Fulani kuwaongoza watu waache njia zao potufu na kufuata njia njema na za haki. Mitume hutumwa pale ujinga na giza linapokithiri ili kuwapa elimu na muongozo ili waweze kukamilisha kusudi la Maisha yao kama apendavyo Mwenye enzi Mungu mwenyewe.
Masihi ni Mfalme atokaye kwa Mungu kwa ajili ya utawala, ustaarabu na usimamiaji wa Mambo katika siasa, Uchumi na Nyanja mbalimbali. Kuhusu Yesu Kristo (Masihi Issa) Mungu Mwenye Enzi alikusudia kufunga na kuhitimisha enzi ya Watoto wa Israeli kama Wateule na Vipenzi na utakuwa umegundua kuwa Hakuoa wala hakuacha Mrithi bali Mamlaka yake aliyagawa kwa Wasaidizi wake na Wafuasi. Masihi ni Hekima, Masihi ni Falsafa, Masihi ni Mfano, Masihi ni Mtesekea Sheria, Mrahisishaji wa Sheria kwa Hekima kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Kujilinda ni kutii na Kufuata. Hekima za wenye hekima dhidi ya Masihi hugeuka Upumbavu
Je wewe tunabishana kuhusu Mambo na hesabu za dunia hii ya leo, Je nikiongea mambo ya Mbinguni utanielewa?! Niliwahi kusikia tuhuma mahali kabla ya Kujitambua kana NABII kwamba watu wanafanya mambo kama watakavyo kwanza halafu wakihojiwa wanajitetea kwa vifungu vya kidini (Qur’an), kuna Mwanafunzi mwenzangu aliuwa tabia yangu ya Ubishani wa kidini na Wanazuoni wa Kiislam kwa kauli yake ya “Alipo Shelimo (Ahmad) kuna ubishani” isivyo bahati alipata Ajali ya Gari na kuvunjika Mguu akiwa pamoja na Kijana wa kichaga aliekuwa anatishia kuniuwa na kunipiga kisa ya Ubishani wangu na Wakristo na kunipiga marufuku kusomea Bwenini, huyu yeye alifarika katika Ajali hiyo.
Nisiwachoshe Karibuni:-
