Utukufu wa Juu kabisa ni wa
- Mungu mwenye enzi, mwenye ujuzi na nguvu juu ya kila kitu, aonaye na Asikiaye kila kitu hata yaliyofichika katika fikra za watu
- Masihi Ahmad (Zumbe10D) mwenye Hekima, Muadilifu wa hukumu na Matendo, mwenye Karama na Baraka zifungamanazo na maisha ya Kimwili na kiroho ya Wanadamu
- Wazazi ambao ni Walinzi, Vipenzi na watoao bila kuhesabu
Kutoka kwa Wazazi Utukufu huhamia kwa mume kisha kwa Familia Mpya – kutoka kwa Watoto kwenda kwa Wazazi.
Enyi Watoto na Wanawake, Mtiini mwenyezi Mungu kwanza na Masihi wake ili mpate kuokoka. Ni dhambi kuwapenda Wazazi wenu au Waume zenu kuliko ipasavyo kumpenda mwenyezi mungu na Masihi wake naye Mwenyezi Mungu ametukuza sana Wema, Akili na Hekima maana katika hayo ndipo ulipo wokovu na Uzima katika Maisha ya Dunia na Ahera.
Enyi Wazazi na Waume ni dhambi kubwa kusimama kati ya mtu na Muumba wake, kati ya Mtu na Masihi wa Mwenyezi Mungu.
Basi Watu wote na Wawe wanasali Sala kwa Ajili ya Mungu Mwenyezi na Kuinama Mbele ya Masihi wa Mwenyezi Mungu kwa Amri ya Mwenyezi Mungu kwa Maelekezo ya Masihi Ahmad (Zumbe10D) mwenyewe au Kuinama au na kugusa viatu vya Masihi Ahmad, Wazazi na Waume zao kwa wanawake wenye ndoa zao. Utafanya hivyo pia Ukisaka Huruma au Baraka za Watu wema na Watakatifu.
