Zumbe ni neno la Kisambaa, Miongoni wa Lugha za kiasili za watu wa Tanzania ambayo wengi wa wazungumzaji wake wanatokea wilaya ya Lushoto na Korogwe Mkoani Tanga. Zumbe ina maana sawa na neno Mfalme au Sultani. Mimi Ahmad kama Wa awali katika Juhudi na Kusudi na harakati ya uanzishwaji wa Taifa Jipya ndani ya mataifa nimeamua kutumia jina hilo kama jina (“Brand”) la nyumbani kuweza kutofautisha Falme yangu ninayoianzisha na Falme zilizopita / Zilizopo. Falme yangu Haina uhusiano na mila na Tamaduni za Kisambaa au Falme zake za kale, Ila kama falsafa yenyewe itakavyo siachi kuheshimu Hekima zitokanazo na Tamaduni na Falme hizo.
Muunganiko wa Maneno matatu
Zumbe10d inatokana na maneno matatu, Moja la Kisambaa na Mawili ya Kiingereza. Neno Zumbe linamaana ya Mfalme au Sultani, Neno Ten na dii ni maneno yenye asili ya Lugha ya Kiingereza, Ten hutafsiriwa kama Kumi na inaweza kuandikwa kwa tarakimu 10,
Neno “dii” ni Silabi D ambayo ni kifupi cha neno Dimensions ambalo laweza kutafsiriwa kwa Kiswahili kama Upeo (mwingi).
10D inahistoria ndefu kidogo, Kabla ya kutumia 10D nilikuwa najiita “10D Thinker” yaani Mtu awazaye katika Upeo wa 10.
3D (Three Dimensions)
Labda ifahamike tu kuwa kwa kutumia macho kuangalia kitu (Hususan kwenye Sikirini) utakiona katika upeo wa 3d na mara nyingi walimu huwahimiza wanafunzi wawaze katika 4D, hiyo D ya nne iwe Zaidi ya kile walichoona. Lilikuwa Jambo la kawaida Darasani kwetu kuwa Mjiolojia analazimika kuwaza Zaidi ya 3d. Wakati huo wa 2009 / 2010 kilikuwa kipindi ambacho nilikuwa na changamoto za Kiroho na Kimaisha maana licha ya Tabia na Mwenendo wangu mwema na kuchukia upweke bado sikuishi maisha ya urafiki wa kweli wenye tija na yenye Ushawishi wenye Manufaa. Na lilikuwa ni Suala ambalo haliingii akilini kuwa napaswa kubadilika Kitabia na Kimwenendo ili niweze kufanikisha hayo. Na ndio maana baadhi ya wakati baadhi ya harakati zangu naziita “Harakati za Kibishi” maana siko Tayari Kubadilika kitabia na Kimwenendo kwa sababu ni Mzuri na Mwema
- Kwa hiyo:-
- Zumbe : Mfalme
- 10 : Kumi
- D (imensions) : Upeo (mwingi)
Mambo ya kuzingatia
Zumbe10D kwa Kiswahili inaweza kutafsiriwa kama “Mfalme Mwenye Upeo Mara Kumi” nasema kuwa inaweza kutafsiriwa maana hilo sasa ni JINA na haipaswi kutafsiri Jina hata ukibadilisha lugha ya Mazungumzo. Kwa sasa hilo ni Jina langu na Jamii yake itaitwa jamii ya Zumbe10D

