Ni lazima kusali Sala ya Asubuhi na sala ya Jioni kila siku, katika sala hii mkusudiwa ni Mungu mkuu mwenye enzi yote, Sala hii ya Asubuhi na Jioni husaliwa kwa Rakaa mbili, Maneno yote yasomwayo kwa sauti yaani Qur’an na Muongozo wa Imamu yanasomwa kwa Kiarabu na maneno ya Kimya yanasomwa kwa lugha aifahamuyo vyema huyo anayeswali.
Sala ya Asubuhi husaliwa asubuhi kabla ya Jua kuchomoza au mara tu baada ya kuamka asubuhi, Sala ya Jioni husaliwa baada ya Jua kuzama au mara tu apatapo wasaa kabla ya kulala.
Ni lazima kuchukua udhu kabla ya kusali na Masharti ya udhu ni kama waelekezavyo Wanazuoni wa Uislam ule tulioukuta usiopingana na Maelekezo yaliyo katika Qur’an. Utaosha viganya vya mikono, eneo lote la uso, mikono hadi kiwikoni, kupaka maji kichwani (Sehemu ya mbele au kichwa chote) na kunawa miguu hadi kifundoni (Sio gotini)
Baada ya Sala itafuatia Sala ya Ufalme, Hii husaliwa kwa kupiga magoti na kusoma mwanzo hadi mwisho katika lugha ya Kiswahili.
Sio lazima kuelekea Kibla lakini ni lazima kuheshimu kibla ukiwa katika Misikiti ya Waislamu wengine kuheshimu enzi na Historia njema.
Sio lazima Kuoga Janaba baada ya kufanya mapenzi na Mkeo kabla ya sala, lakini ni muhimu kujisafisha maungoni (Sehemu za siri) na kujifuta maeneo jirani kwa nguo yenye unyevunyevu na kujikausha
Sala ya Asubuhi ni lazima isaliwe ndani ya Familia kwa kuongozwa na Baba au kijana wa kiume aliepewe ruhusa na wazazi kwa kauli ya Baba. Sala ya Jioni Husaliwa pamoja na Majirani na kuongozwa na Mwanaume katika wao ambaye ni muadilifu na mboboezi katika Imani Yetu
Mtaa mmoja lazima uwe na Sala ya Ijumaa moja kwa Walio katika Imani Yetu. Wanaoasi au kufuata mwenendo usio wetu watatengwa kwa Ijumaa mbili na kisha watarudi kama waumini wa kawaida na sio waongoza Ibada wala Wafundishaji.
Sala ya Ijumaa ina hotuba mbili, ya kwanza ni juu ya Ibada na Wema katika namna mbalimbali na hotuba ya Pili ni umuhimu wa Falme ya Ahmad kwa Waumini na watu wema kupata urahisi kwa mambo yaliyojadiliwa katika hotuba ya kwanza
Ni lazima kwa Wanawake kufunika vichwa vyao katika kila sala na sio makosa kuacha wazi viungo vyote vya udhu ikiwemo sehemu ya mbele ya nywele zao
Kiwepo Kiti Maalumu Cha Masihi Ahmad mbele ya Chumba / Nyumba ya Ibada ambacho kimefungwa kitu juu kuzuia wengine kukalia kwa Makusudi au bila kujua.
Baada ya Sala ya Asubuhi / Jioni / Ijumaa itafuatiwa na Sala ya Ufalme kwa Kiswahili.
Kwenye Chumba cha Ibada ni lazima Iwekwe picha kubwa ya Masihi Ahmad (Zumbe10D) ambayo imefunikwa na Pazia wakati wote wa Sala kwa Mungu mwenye enzi na kufunuliwa wakati wa Sala ya Ufalme
Kiti cha Masihi Ahmad kitakaliwa na Masihi Ahmad pekee katika Uhai wake Kisha Mrithi wake, kisha mrithi wake hadi Kiama.
Ni Jambo zuri kusikiliza Audio za Wasanii / Washairi bila kucheza kwa dhumuni la kupongeza kazi zao au kuzipiga Marufuku kwa Waumini wote. Mengini ni Mambo ya Aibu sana kwa hiyo Itatangazwa Misimamo Kwenye Nyumba Takatifu ya Zumbe Ten’dii (Nyutazute) na Waumini kwa Muda wao wenyewe watasikiliza mtandaoni na kuacha huko huko. Tutukuze Wasanii / Washairi wetu bila kuingiza vyombo vya Muziki kwenye Nyutazute.
Audio nzuri zitakataliwa kama Video zake hazizingatii uvaaji au kuhimiza Mambo ya dhambi na kushusha heshima ya Kusudi la Zumbe10D na Falme ya Ahmad (Taifa Jipya), Na hili litagusa kazi nyingine za Video vile vile

