Haya ni Malengo shabaha ya Utawala wa Zumbe10D na wala sio ushawishi kwa watunga sera. Falme ya Ahmad inakusudia kumiliki kila kitu bila kukichukua, na kuunda umoja ambao sio wa kunyang’anyana bali wa kugawana.
Pata picha hii, Hakuna Matumizi wa Fedha duniani kote na hapo utagundua ya kuwa mambo ya wizi na utapeli vitakuwa ni vitu ambavyo vinawezekana kwa tabu sana na kwa tendo hilo tutakuwa tumewakatisha tamaa kundi kubwa na walaghai na matapeli.
Mali za maghalani na viwandani nazo tutazigawa bure kwa watu kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo, hapo tutakuwa tumeondoa umaskini ambaye ni mama wa Madhambi mengi sana na uduni katika maisha ya mwanadamu. Umaskini utashindwa kuvunja ndoa za watu,
Watoto wadogo watapenda heshima na utukufu ufaao kutoka kwenye malezi ya wazazi, walimu na Viongozi wao wa Dini ambao wanastahili heshima yetu kwa kule kulinda uhalisia.
Wanawake watakuwa wanaolewa kwa sababu zilizotukuka na sio tamaa ya vitu au kinga ya Umaskini. Watapata mavazi bure, sehemu za kuishi bure, vipodozi bure. Wanawake wanapokuwa wanajitosheleza, kujikombakomba kwa wenye pesa hakutakuwepo na jamii yetu yenye falsafa ya Mashariki haitaruhusu uzinifu.
Ndoa ni ibada itukuzwayo sana kitaifa – na hapo itawafanya wanaume wapende utukufu na heshima ifaayo ya kuchaguliwa wao na wanawake wale ambao wanasukumwa kwenda kwenye ndoa kwa mapenzi safi / Salama / mema na matukufu.
Mwanamke kuchagua umalaya katika mazingira ya Taifa jipya inahesabika kama tamaa ya kuvuruga utaratibu uliopangwa vizuri wa Mashariki ambako maisha yamepangwa toka utotoni hadi uzee.
Watu watapewa Nyumba kadri ya ukubwa wa familia na matumizi yao yakubalikayo kitaifa. Na kwetu Mtoto aliyebaleghe inampasa kupewa chumba chake peke yake na akipata mwenzake (Mume / Mke) inapaswa kupewa vyumba vitatu au Zaidi. Na hili linafanyika kupitia sera ya kujenga taifa sisi wenyewe kwa mawe yetu, simenti yetu, mchanga wetu na mabati ya chuma chetu wenyewe.
Na wazee na watu wazima watajengewa makazi yao bila kuondosha nafasi zao ndani ya familia zao. Watakuwa huru kwenda na kurudi kwenye Makazi hayo au kutumia baadhi ya masaa ya siku kwa ajili ya kujifurahisha au kujipatia huduma kwa urahisi
Kwa mpango huu wa Makazi nitauwa ndege watatu kwa jiwe moja – Watoto wa kiume wakubwa na wadogo watanusurika na Ushoga, sera yetu inakubali ndoa za mapema na ndoa sio mwisho wa masomo, Watoto wetu wa Kiume kupitia upendo wa watoto wetu wa kike watajifunza mapenzi kwenye ndoa zao na kusawazisha usawa kwenye Jamii ya wanaume na Jamii ya Wanawake.
Dunia hii ya Taifa la Kifalme haitaruhusu wanawake kuwa viongozi wa Kisiasa na hapo tunafunga mchezo wa wanafiki waabudu Jicho (Wasenge) kupata mashiko kwenye jamii yetu mpya.
Napenda wale ambao wanafuatilia lengo shabaha hii wajue kama Mashamba ni ya Taifa; basi taifa ndio litalima mashamba hayo – kuwa mkulima ni heshima na hatutaruhusu uwe mzigo.
Serekali italima, kuchimba na kuvua malighafi, – itazipeleka viwandani – itazichakata huko na kuzifanya tayari tayari – na kisha itazisambaza kwenda kwa raia wake.
Dunia ya leo Ajira ni tatizo, na kwa minajili hiyo umaskini hautaacha kuandama watu. Fulu stop.
Ni ukweli uonaishi kwamba nafasi za kazi za kuajiriwa au vibarua ni chache sana. Fulu stop.
Jambo hili ni homa ya mataifa lakini kwetu ni neema. Fulu stop.
Sio lazima wote tuwe kazini kwa wakati mmoja kwa lugha nyingine inabidi wote tufanye kazi. Kazi kwa zamu. Na hapo utaona mwanzo wa Mapunziko makuu na mema ndani ya Maisha ya wanadamu. Ajira zitapungua sana. Mambo ya Pesa na biashara yote yatakwenda kwenye timu ya Usambazaji.
Wote tutafanya kazi – Kazi ni chache sana – Subiri zamu yako – Kazi kwa timu – Timu na Kiongozi wake – Mambo kielectroniki – Kila mtu ananamba yake kama namba ya Simu / Utaifa (NIDA)

