Kwaheri Ramadhani
Nimakosa kuuita mwezi wa Ramadhani mwezi wa toba, Ramadhani ni mwezi wa upendeleo utako kwa Mungu mwenyezi kwa waja wake. Lengo la Ramadhani limewekwa wazi – Tuwe wachamungu.
Uchamungu ni Zaidi ya kuwa muumini ambapo uumini ni Zaidi ya kuwa Muislamu tu. Yale yote uliyoacha ndani ya Ramadhani ukiachilia kufanya mapenzi na Mkeo / mmeo mchana na kula mchana, ukiyafanya kwenye miezi mingine bado yanakutoa kwenye Uislam
Hakuna ruhusa ya kuiba, kusengenya, kuzini, kufitini na makossa yote ambayo yameanishwa vyema kwenye kitabu cha Qur’an – Karibuni kwenye Podcast
Kuna watu wameacha kunifanyia mabaya kwa sababu wanaogopa laana zisababishazo hadi kifo – Wapo wanaonifanyia mabaya kwa sababu wanajua laana zisababishazo kifo huenda kwa watu wengine. Sitaki kuchezewa, mwisho wa siku nao laana zitawauwa kwa sababu wao nao wamekuwa wabaya.

