Zumbe10D na Psychosis
Nakutana na changamoto nyingi sana kwa kisingizio kwamba nina matatizo ya afya ya Akili, Changamoto hizo zinapelekea suala la uchumi wangu kuwa duni na duni kila siku. Napaswa kufanya kazi na kuwa na kwangu kwa maana ya nyumba na kwangu kwa maana ya Familia, Naishi bila mke na sina cha kusema zaidi ya kulaumu hali yangu ya kiuchumi lakini pia uhusiano wangu wa kijamii unaoharibika kwa sababu ya kashfa ya Ugonjwa wa akili.
Ni jambo la ajabu sana kufanya mapatano na mgonjwa wa akili aliye Wodini iwe ndio kigezo cha kutoka. Hapa tunazungumzia mgonjwa wa akili. Kwanini hawanipeleki ofisini kama kuna mikwaruzano ndani ya familia?! Mama aliwahi nijibu kuwa “Wengine tunauwezo mkubwa wa kujieleza” na ndio maana hajaribu huko.
Mimi ni mwanaharakati wa kiimani, napambana na unyonyaji wa kila aina na nimekuwa tishio kwa maslahi ya baadi ya wanajamii. Napigania usawa wa fursa za kiuchumi na mgawanyo wa keki ya taifa.
Napambana na mifumo ya uchumi na nimekuwa changamoto ya kweli kwa watu wa dini mbalimbali huku nikiunda jamii ya Waislam wa Y2K au Wanyenyekevu.
Kumuingiza Kikwete ikulu ilikuwa ni makosa makubwa sana kwa falsafa na mila zetu kwa waafrika wa Tanzania na mseto wa dini zetu. Mambo mengi sana ya Kisenge yaani ya mabasha na mashoga yalipata mashiko ndani ya jamii yetu. Naamini kabisa Sheria ya kuwapeleka watu kukaa wodi za wagonjwa bila kupata ridhaa yao na bila kupitia kibali cha Mahakama “Kwa kumsikiliza kwanza Mtuhumiwa/Mgonjwa” iliondolewa wakati wa utawala wa kikwete
Nilipoongea wengi hawakuelewa lakini sasa wapo wengi sana wanapenda baadhi ya sheria zilizopitishwa wakati wake ziondolewe wapate nafuu – wanashindwa kuoanisha kwamba zipo kwa ajili ya kuinua na kulipa kundi moja ushindi na uhuru kwa gharama ya maisha na uhuru wao. Waliona mambo hayo hayawagusi na kila msimu na mambo yake
Daah!! Kwenye Pod kuna neno Baba Mlevi, sijui limeingia vipi neno hilo, ni Baba Mlezi, tena yuko mbali kweli kweli na tabia za unywaji wa pombe. Naomba radhi kwa usumbufu wowote kwa maana siwezi kuirudia leo hii kwa ernegy ile ya siku ile.

