Leo tunasimama katika hatua ya kihistoria: mfumo wa kushughulikia taarifa za wanachama wa Zumbe10D umekamilika kwa asilimia 100. Hii siyo tu kazi ya kiufundi, bali ni ushuhuda wa dhamira yetu ya kujenga jamii yenye heshima, usalama na mshikamano wa kweli.
Huu ni Wito kwa kila mtu kujiunga na jamii yetu pendwa .Tunawaomba wote wenye moyo wa matumaini na heshima wafanye hima kujiunga. Bofya hapa kujiunga
Mazingira Pendwa na Salama
Kwa mara ya kwanza, wanachama sasa wanaweza:
- Kuweka machapisho kama ilivyo kwenye mitandao ya kijamii.
- Kujenga mazingira pendwa na salama ndani ya jamii ya Zumbe10D.
- Kuishi na kushiriki katika maisha haya au maisha yajayo, kwa pamoja au kwa namna ya kipekee. Hii ni nafasi ya kuunganisha siasa moja na ufuasi wa kidini, au siasa safi za mambo yetu katika uhai huu wa sasa bila kufungamana imani za maisha yajayo
Maono Yetu
Zumbe10D siyo tu mfumo wa mtandaoni. Ni jamii ya kiroho na kisiasa, inayojali:
- Ibada na imani kama msingi wa utu.
- Familia na heshima kama nguzo ya maisha.
- Sanaa na michezo kama pumzi ya furaha na ubunifu.
- Siasa safi na ufuasi wa kidini kama mwongozo wa uhai wa sasa na uhai wa milele.
Karibu
Hii ni mwaliko wa dhati: Karibu kwenye Zumbe10D. Karibu kwenye jamii ya matumaini, usalama na heshima. Karibu kwenye harakati ya kuandika historia mpya ya maisha haya na yajayo. Bofya hapa kujiunga

