Zumbe10D niko kamili, Niko na mifumo mingi sana kwa ajili ya kuchukua nafasi ya hii inayotumika ambayo hupelekea mahangaiko kwa Binadamu. Lengo langu ni lile lile na kuifanya dunia tulivu na yenye raha na starehe za kila aina na kwa kila mtu
Kabla sijaanza kuufafanua mfumo wangu ningependa kujadili kuhusu taaluma ya ubobeaji (Professionalism). Wataalam waliobobea ni muhimu sana katika ufanyaji wa kazi na oparasheni mbalimbali. Mfano Madaktari wanaanza kujifunza kuhusu Viumbe wote, Kisha Mwili wote wa Mwanadamu, kisha ataegemea upande Fulani wa mwili wa mwanadamu. Yaani kuna daktari ya Masikio, Daktari wa Meno na Daktari wa macho nk. Na huo ndio ubobeaji
Mifumo iliyopo ya elimu ni mipana sana katika kuelimisha Mwanafunzi Mmoja na inachukua Muda mrefu Sana kumfanya Mbobeaji. Watoto wanaanza kujifunza Masomo kumi au zaidi Sekondari, Kisha masomo matatu Sekondari ya upili (high school) na kuchagua kozi Fulani chuo kikuu na hapo bado hajafika ubobeaji.
Mtoto anaanza shule na miaka sita au saba darasa la kwanza, akifika darasa la saba na kumaliza atakuwa na miaka 13 / 14, ataenda sekondari na huko hasomei kazi yoyote bali kujazwa maarifa mbalimbali, anapewa elimu yeye msingi wa kila taaluma uijuayo dunia, yaani atasoma Kingereza, Chemia, Biolojia, Jeografia, Historia, Hesabu, Uraia, Kiswahili na masomo mengine kama kilimo, Biashara, Uchumi au Ufundi
Elimu hiyo imekaa kikoloni sana, inalenga kuwapitisha watu kwenye jamii na nchi kwenye mchujo mkubwa sana. Elimu hiyo inahangaisha, ili ufanikiwe lazima uipe maisha yako yote, inakera sana na ileta hata msongo wa mawazo, Elimu hiyo ni kandamizi maana inataka wahusika waachane na Starehe na uzalishaji mali ili waipe muda wao wote.
Kijana akimaliza sekondari ya awali atakuwa na miaka 17 / 18, akienda sekondari ya upili atamaliza na miaka 19 / 20, baada ya hapo ataenda kusomea kazi akiwa chuo kikuu.
Matokeo ya darasa la saba, Sekondari ya Awali au ya upili hayawezi kumpatia mtu kazi, labda apachikwe baadhi ya sehemu kusaidia baadhi ya kazi.
Elimu tuliyonayo ina asili ya piramidi, Jinsi unavyosonga mbele ndivyo inavyo watupa au kupukutisha watu wengi nje ya mfumo rasmi wa elimu na kubakia wachache na ndio maana hata udhamini wa degree moja ni kidogo sana kuliko ule wa degree ya pili, Mfumo unajilinda usianguke, unawafanya wasitosheke na Degree moja. Degree ya kwanza huchukua miaka mitatu hadi mitano, kwa hiyo anatarajiwa kuhitimu degree ya kwanza na umri wa miaka 22 hadi 25, Hapo sasa ndio anapumzika kusoma aende kazini, na kazini nako atakuwa ni kuwasaidia wabobeaji wa taalumu husika au kuachiwa mambo ambayo hayahitaji ubobeaji.
Na kwa tamaa ya mishahara mikubwa wengi huamua kurudi shule tena. Wako busy na masomo, hawako busy na mume / mke wala watoto, hao watalelewa na mayaya au shule za Bweni. Kuhusu mume au mke atachepuka bora ajifiche mwenzie asijue, Ni upuuzi ulioje?
Mfano Nilioa na miaka 26 na bado wanazuoni wenzangu wananiuliza mbona nimeoa mapema.
Dunia ni nayo ijenga ni ya Starehe na Burudani kwa kila mtu, Hakuna kuwaza kuhusu utajiri maana kila kitu unaletewa hadi mtaani kwako na vingine vya jumuiya utavitumia kama vyako zamu yako ikifika, rejea chapisho langu la “Usawa na Utajiri duniani”. Dunia ya Mapenzi ya jinsia tofauti na yaliyo rasmi tangu balehe katika mazingira mazuri na salama. Kazi zitafanywa na mashine na mashine zinahitaji wasimamizi na ndio hao tunaopeleka shuleni, wabobee kweli kweli kwenye Mashine zao na kazi yao
Mtu akishamaliza Elimu ya Msingi basi atachagua taaluma yake ya kubobea. Wanazuoni wetu wa zama hizi watapangilia kila kitu kihitajikacho kwa ajili ya ubobezi wa taaluma Fulani, atasoma miaka kama miwili au mitatu na kumaliza. Tutapata wataalumu mfano, Mtafuta dhahabu, Mchimbaji Almasi, Daktari wa Meno nk. Ikiwa Elimu ya Msingi Ni miaka mitano au sita jumlisha na Miaka mitatu ya Ubobeaji itakuwa nane au tisa na aliyeanza darasa la kwanza na Miaka Saba atakuwa na Miaka 15 au 16
Kusoma muda mrefu ni kwa kazi gani? Mnataka kuwageuza Encyclopedia?
Kutakuwa na tovuti rasmi mithili ya “Alson online certification” kwa ajili ya watu kujiongezea maarifa wanayo hitaji nje ya taaluma zao za ubobeaji.
Watu wanatafuta kazi, nitawapa kazi wote, na kazi hazitoshi watapeana zamu. Ni mwendo wa Starehe na Burudani njema iliyotakaswa. Ni kula na kunywa kwa Afya zaidi
