Usawa Na Utajiri Duniani

Zumbe10D ndio mfalme wa Dunia ya kidijitali na ameigeuza kuwa Bustani ya neema. Hakuna Maskini hata mmoja. Umaskini ni suala ambalo liko katika historia. Dunia isiyotumia fedha, Dunia isiyo na Wafanyabiashara bali nafasi yao itachukuliwa na Timu za Usambazaji. Mahitaji yatakuwa yanagawanywa kuwa kuzingatia umri na hali ya mtu.
Nyumba za maana kama zile za “Marehemu” Dege Village zitagaiwa kwa Wananchi kwa mujibu wa hali zao za Ndoa na Rika. Kuna makazi kwa ajili ya Vijana wenye ndoa changa na wale wenye familia. Familia ikiwa kubwa na watoto hawakidhi vigezo vya kupewa makazi yao basi itabidi wahamishiwe kwenye nyumba kubwa, Japo napenda sana uzazi wa mpango, kwa ajili ya afya ya mama na mtoto, Mwenye sipendelei kujipangia idadi ya watoto bali umri wao wa kupishana, napenda sana ikiwa ni kwa Zaidi ya miaka mitatu
Siri ya Uchumi wa zumbe10d ni Uaminifu na utiifu wa walimwengu kwa familia tukufu ya Zumbe Ahmad Ten’dii wa Lukozi Lushoto (Wakati wa Chapisho hili mimi Ahmad Ten’dii ni Mkazi wa Yombo Vituka Dar es Salaam).
Nitasimamia upatikanaji wa Malighafi za Viwanda na jinsi ya kuzifikisha viwandani malighafi hizo na usambazaji wa Bidhaa zinazozalishwa na Viwanda hivyo.
Kwa mfano, Viwanda vya Kompyuta vinahitaji Madini mbalimbali kama dhahabu, Nikeli, Shaba nk. Basi amri itakuwa yachimbwe kwa ufanisi wa hali ya juu na yakabidhiwe kwenye Viwanda mara moja. Watuzalishie Kompyuta za hali ya juu baada ya kuchanganya Teknolojia za huku na kule, Hakuna kuzalisha bidhaa za viwango wa chini (Vya bei nafuu). Kisha zitagawanywa kwa Raia na kuleta usawa. Hiyo itahusha viwanda vyote vya Elektroniki yaani simu, TV, Kamera nk. Na utaratibu huo utatumika katika kila Sampuli ya Viwanda.
Trekta ngapi zinatosha kulima mashamba ya kata nzima kwa Mwezi? Wanahitaji Madini ya aina gani na kiasi gani kutengeneza trekta za kutosha? Basi yapelekwe. Wanahitaji wafanyakazi kiasi gani wapatiwe?
Kila mtu atapewa jukumu la kutimiza kwa mujibu wa Elimu yake, Rika na Hali yake.
Wengine wataenda kuvua kwa meli kubwa, Mchanganyiko wa Wataalamu na Wasaidizi, wanarudi na Samaki tele maana wanazifuata hadi kwenye kina kirefu. Samaki wakiwa bado wabichi watawekwa kwenye makontena na kusambazwa na timu ya Usambazaji
Aridhi yote itakuwa ya Mfalme, Kuna watu wataaminiwa kufanya kazi za shambani chini ya usimamizi maalumu, Mazao yakishavunwa yatapelekwa kwenye maghala ya mfalme tayari kwa ajili ya kusambazwa bure kwa raia
Kazi karibia zote zitafanywa na mashine kuanzi upishi, ufuaji, ukulima, ubebaji na kadhalika
Kipindi hicho na kiona kama kipindi ambacho watu wengi sana watakosa kazi, na hilo sio jambo la kulaani bali jambo la kufurahia na kusherehekea. Kwa ajili ya usawa watu watafanya kazi kwa zamu kwa mujibu wa taaluma zao.
Sanaa itasafishwa na kupewa hadhi ya juu sana, Maana dunia hiyo ni dunia ya starehe, Watu watatumia muda mwingi kwenye starehe Zaidi kuliko kufanya kazi maana kazi ni chache na zimekabidhiwa kwa mashine na zinahitaji tu waongozaji. Na hakuna ambaye atakuwa hafanyi kazi, Kwa hiyo hizo kazi chache zitafanywa na watu wote.
Watu wanataka kazi, nitawapa kazi.
Ufame wangu ni ufalme wa Utajiri kwa kila mtu, Madaktari watatibu Bure, Wachimba mafuta watachimba bure na Kusafiri itakuwa bure hasa kama umeshakamilisha taratibu zote za eneo lako la kazi (Kazini)
Kila kitu ni Bure, Kuanzia nyumba ya kuishi, Masomo, matibabu, mawasiliano, chakula nk. maadamu tu hujajitoa katika utiifu na uaminifu kwa mfalme
Ndoa tangu balehe hadi unakufa. Taasisi ya ndoa itawekewa Sheria mahsusi ili ing’ae na itukuke kwa heshima, Kila mwanaume ajikute Mfalme kwenye mji wake na Mkewe / Wakeze ajikute / wajikute Malkia
Ushaawahi kusikia kesi za Uhaini ngazi ya familia?! “Fulani na mke / mume wa Fulani wamekula njama kuporomosha staha na heshimu ya familia ya Fulani kwa kuanzisha uhusiano kizinzi wakati wakitambua mapinduzi kwenye Falme za familia hayapewi nafasi na Mfalme (Zumbe) Ahmad Ten’dii”. Kama mmechokana peaneni talaka iwe halali kwa wengine, Hakuna kuchakachua.
Sasa tazama hakuna Kujipinda kupata mali au utajiri, Hakuna kuteseka sababu ya Kimapenzi au uduni wa Ushoga? Kila kitu umeshafanyiwa na Mfumo wa Mtukufu Zumbe Ahmad Ten’dii.
Kujiunga na taasisi na jumuia za Zumbe10d kisiasa ni Ushujaa na Upendo kwa wakazi wa Dunia, Watoto wetu na Vizazi vyetu. Rahisi namna hiyo.
TV ndogo zitakuwa za kazi gani sasa?! Aaaaaaa! Za kuweka kwenye magari, sawa sawa. (Mara utasikia hiyo ndogo naitaka. “Hapana utapewa kubwa ya kupendezesha sebule lako”)
Ni somo rahisi haihitaji “tuisheni” kunielewa
Pia nakaribisha wafuasi wa kidini, Karibuni sana