1. karibuni katika jumuiya Zumbe Ahmad Ten’dii.
  2. Mnaweza kuunda vikundi vya watu chini ya Ishirini. Idadi ya Wana Kikundi ikifika 15 au zaidi mtaruhusiwa kuwa na kiongozi wenu.
  3. Kwa mara ya kwanza utaruhusiwa kujiunga kama mwanafunzi au mdadisi
  4. Ndani kuna Blog ambayo Kila Aliyejisajili anaweza kuweka Machapisho yake katika Mada zinazohusiana na Kundi, Jumuiya au Safari ya Taifa Jipya na Mambo yapatikanayo katika Shule yangu ya Mawazo na Falsafa
  5. Baadhi ya mambo hayatafundishwa kila mtu isipokuwa watu waliojisajili katika tovuti hii
  6. Ili mtu atambulike kama Mwanachama lazima anunue stika ya utambulisho
  7. Kwa sababu moja au nyingine watu kwa Ruhusa Maalum wanaruhusiwa kujiunga kama watu wasiojulikana na watu hao watawekwa katika kundi moja na alama kuwatambulisha.
  8. Baada ya wiki tatu Mwanafunzi au Mdadisi anaweza kuomba kuhamishiwa kwenye kundi la Wanachama
  9. Kuna mambo ambayo yatakuwa hayapatikani kwa wanafunzi na wadadisi. Yatapatikana kwa wanachama na viongozi wao
  10. Wanachama watasikiliza Podcast (Vipindi midhili ya Redio Mtandaoni) na kusoma Machapisho ya Kulipia Bure
  11. Kuwa mwanachama inabidi uchangie Shilingi Elfu tatu kila wiki
  12. Mnaweza kuunda kikundi cha wanafamilia au marafiki mtaani au Mnaopatana na kuwa Karibu kwa Msaada ya Teknolojia
  13. Tabia za Kihalifu, Ushenzi na kupuuza Tabia Njema na Ustaarabu kama ziruhusuwazo mitandaoni, sheria za kimataifa na Mila na Desturi zetu Hazitavumiliwa.
  14. Mabishano ya Kidini hayatapewa Nafasi na kuendelea Baada ya Onyo la kiongozi utafungiwa au kuondolewa kwenye kundi
  15. Ni Ruksa kuhitaji “Ridhaa tukufu” katika Mijadala ambayo itaibua Mazogo bila Maelewano Kwangu Zumbe10D.