Mimi Ahmad Ten’dii naanzisha Mfumo, Naanzisha utawala wa kutawala Bustani ya Upendo, Bustani yenye hadhi na heshima stahiki, Bustani ambayo Mwanadamu atachanua na kunawiri katika Nyanja zote, Nyanja zenyewe zitakuwa chache maana maisha nitayaelekeza katika uhalisia wake na sio nadharia zake
Bustani hiyo Wanawake watafurahia asili yao na Wanaume watafurahia asili yao, Wanawake watajivunia asili yao na Wanaume watajivunia asili yao. Humo ni kula, kunywa, kustarehe na kuburudika
Watu wa Dini za Mungu wanakaribishwa kwenye utawala huu na hawatachukuliwa tofauti kwa namna yoyote ile – “Karama” zao zitawapatia Heshima kwetu na Imani yao itaheshimiwa na haitabughudhiwa
Wote mnakaribishwa katika ujenzi na ulimaji wa Bustani hiyo na yule ambaye hatashiriki ameamua kujitenga na Maisha na Mavuno yale yatakayopatikana katika Bustani hiyo. Na waliotanguli sio sawa na waliochelewa, waliotangulia hujipatia nafasi na wasaa wa kuchagua pa kukaa ama pa kushika, nadhani mfano huo unaeleweka wazi kwa kila akili huru
Mimi Ahmad Ten’dii natumia maneno laini ya kukuomba wewe peke yako kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Utukufu wa Ufalme wangu, Vile vile nakuomba uishawishi familia yako na watu wako wa karibu au wale wote unaoweza kuwafikia wawe waaminifu na watiifu kwa Utukufu wa Ufalme wangu Mimi Ahmad 10D
Nilisema mwaka 2010 tuifanye dunia kuwa Bustani na mvua za neema na aridhi itatoa mazao kwa rutuba yake nzuri basi tuifanye Dunia bustani yaani upandaji wa miche ya Matunda na ujenzi maadam mimi Masihi nawahakikishia hilo
2017 – 2022 nimewaambia nami mtukufu Ahmad Ten’dii nilipaswa kuwa Mnufaika kama Mfalme na kiongozi wa Dunia hiyo ambayo nilitoa muongozo wa jinsi ya kuijenga, Dunia haikufikia lengo langu kwa sababu ule ukweli wangu waligeuza kuwa upuuzi na upuuzi wao wakaugeuza kuwa ndio ukweli wa Muongo. Tangu wakati huo hadi sasa mimi nikiwa “Masihi Binafsi” Masihi wa Mimi Mwenyewe nisietaka jina hilo bali “Zumbe”, Zumbe Ten’dii ambaye sifungamani kiimani na Dini za Mungu bado sijabadilika, Safari yangu inaendelea pasina Mungu na ninastahili kuvuna matunda na Fadhila za kazi yangu ya kujitolea kuangamiza Mifumo na Nuru za Bandia na Majitu yake na kuwafanya watu wawe huru na wajuzi kweli kweli
Laana nilizoweka katika Aridhi, Katika Anga, Katika Maji na Katika hewa nitaziondoa, Laana katika Viwiliwili na Afya zake nitaziondoa na neema zitafunguka kupitia Baraka na “Karama” zilizo katika mimi Mtukufu Mfalme Ahmad Ten’dii.
Ni wakati wa Watu kusahau kuhusu Utajiri na Kusahau kuhusu Umaskini. Watakachopaswa kukumbuka ni kuwa Maisha yao ni Bora Zaidi ya Jana. Mkiniita Baba nitawaita Wanangu, Mkinitambua kama Mfalme nanyi mtakuwa Raia wangu
Kila kitu ni Bure Kwenye Bustani, Kwenye Dunia Bustani hiyo Uaminifu na Utiifu wako yaani “Royalty” utalipia kila kitu
Dunia imefikia hatua nzuri, hatua ya kuwa kazi zinafanywa na Mashine, Nikitawala raia watafurahia kukosa Ajira, Kukosa Kazi kama Jamaa zangu wa JWT
Kwa mfano katika Mtaa M, Siku 2 za wiki wanaenda wakazi Wanne wakafue Nguo kwenye Mashine na kuzikausha, Kila familia wafuata Nguo zao (Mwingine atasema “mimi sihitaji hivyo nina mashine tayari nyumbani”, Ndio naelewa pia kuwa wengine hatahizo nguo za kufua hawana). Kisha watarudi kwa familia na jamaa zao kufurahia maisha na kustarehe hadi zamu zao ziwakute tena
Nyie Wakulima, Mlikula wakati usio wa Mavuno, Ninyi na familia zenu mkatibiwa wakati usio wa Mavuno, Mlisoma na kusomesha wakati ambao sio wa Mavuno, Haya Mavuno nayachukua ili kuwalisha ninyi, Madaktari wanaotibu familia zenu na Mainjinia Wanaojenga mji wenu.
Nyie Walimu na Madaktari na Askari na wengineo wote mtapata kazi, Subirini walio zamu wamalize na nyie muende ili na wao wapate nafasi ya kustarehe na kuburudika na washirika wenzao wa familia na Marafiki.
Kuhusu Uvuvi hatupeleki Ndoana Boti wala Ngalawa, Tunapeleka Meli kubwa za Uvuvi, Wale wavuvi wa Boti, Ndoana na Ngalawa sio kwamba watakosa kazi ila watasubiri zamu zao ili wawapokee wale Wavuvi walioko Melini ili warudi kula raha na Washirika wa familia zao na Marafiki. Kwenye Ujenzi, Madini, Usambazaji ni hivyo hivyo nakadhalika.
Shangwe za kukosa kazi zitakuwa Mambo ya Kawaida sana Maana Mashine zinataka waendeshaji tu, Ndio Sio Matrekta tu kuna mashine zinalima kwenye miinuko, unaendesha kama mkokoteni wenye injini na breki.
Karibuni Sana.
