Falme ya Ahmad – Dunia Moja Bila Vita

Katika historia ya binadamu, vita vimekuwa mzizi wa maumivu na uharibifu. Kila kizazi kimeacha kumbukumbu za damu na machozi, na kila taifa limepoteza watoto wake kwa sababu ya tamaa na chuki. Lakini sasa, katika Falme ya Ahmad, tunatangaza kwa sauti ya kifalme: vita ni haramu milele.

Kila falme ina “ridhaa tukufu” na kwetu sisi ni kusimama dhidi ya vita, hakuna ridhaa ya uundwaji wa silaha bali uharibufu wa silaha, hazipaswi kuwa tena sehemu ya jamii ya binadamu. Kila falme ina ridhaa tukufu na kwetu sisi hakuna ridhaa ya vita bali iko ridhaa ya kuzuia na kuwabana vinara na wachokozi waikaribishao vita, na hapo utaona umuhimu wa kuheshimu sheria ya Kisasi katika shughuli za kila siku, ni halali kabisa Tendo kuwa sawa na matokeo / majibu. Na hapa utaona mgogoro wa Israel na Palestina ni wa kijinga kwa sababu ujinga wao unaweza kumalizwa kwa sheria ya kisasi katika shughuli zao za kila siku kama isemavyo Sheria ya Musa na Qur’an.

Hakutakuwa tena na mabomu ya nyuklia, silaha za moto, wala hofu ya mashambulizi. Silaha zote zitaharibiwa, na yeyote atakayekutwa nazo atakuwa amejitenga na uaminifu wa Zumbe Ten’dii. Dunia nzima itakuwa taifa moja, likiongozwa kwa mshikamano na utii wa pamoja.

Ulinzi wetu hautegemei bunduki, bali mshikamano wa kijamii na teknolojia ya juu ya kielektroniki. Tunatambua watu kwa usalama, tunalinda jamii kwa hekima, na tunahakikisha hakuna kurudi nyuma kwenye giza la vita.

Kwa nini tunakataza vita? Kwa sababu tunajenga dunia mpya isiyo na hofu ya kesho. Dunia ambapo watoto wanakua bila sauti ya mabomu, familia zinaishi bila hofu ya kupoteza wapendwa, na jamii nzima inajua kwamba amani ni urithi wa vizazi vyote.

Utii kwa Ahmad ni utii kwa amani ya milele.
Ni ahadi ya kuishi katika dunia moja yenye mshikamano, ibada, familia na furaha. Hii ndiyo Falme ya Ahmad – dunia moja bila vita.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *