Mchango wa Siasa Zetu kwenye Umalaya na Utomvu wa Maadili

Wakati nikiwa mwanafunzi nilikuwa muislamu safi. Miongoni mwa dua zangu wakati huo ni kupatiwa Mke mwema na kipato kizuri pindi nimalizapo masomo yangu. Siku moja wakati niko chuo kikuu nilikwenda baa ya jirani na Geto langu kupata chakula cha Mchana. Meza jirani alikuwepo kijana mmoja na binti, picha ya haraka niliyoipata ni kwamba wanataka kuanzisha mahusiano. Kitu kilichonishangaza ni yule kijana kumfunza yule binti kunywa pombe. Alikuwa akimhimiza anywe kiasi kikubwa na asiwe na hofu yoyote kila kitu kitakuwa sawa sawia. Nilimshangaa sana yule kijana, kwanini anapenda mpenzi wake au mchumba wake awe anatumia pombe. Anaweza hata akazaa naye, sasa kwa nini anapenda mama wa Mwanae / Wanae awe mlevi?!! Baadae nikagundua pombe inaondoa aibu, pia inaleta ulegevu wa mwili kwa hiyo itamrahisishia kushiriki naye mapenzi hata kama hajaridhia kabisa.

Ni kauli za kawaida kabisa mitaani na hata za wasanii wakubwa katika tungo zao kuwa bila Pesa huwezi kuwa na Mpenzi / Mwanamke. Hebu vuta picha Mtu yuko na hela zake halafu hampati yule mwanamke mzuri anayempenda kisa tu mwanamke huyo haweki pesa mbele kwenye kuanzisha mahusiano. Yaani anafuata maadili ya kijamii au ya kidini katika kufanya maamuzi yahusuyo mahusiano yake ya kimapenzi.

Hapo ndipo utakapo gundua kuwa wasanii wanaochechea umalaya na wanawake kujiuza wamekuwa ni nyenzo muhimu sana kwenye kujenga jamii ya sasa. Ndio, Wanawake wajiuze halafu Tajiri anachagua anayemtaka kutokana na hao kisha kwa pesa zake anaweza kumtuliza kwa kumtimizia mahitaji yake yote na kumpa za ziada.

Hapo ndipo yalipo mashindano ya watoto wa kiume kujitahidi kuwa na kipato kikubwa waweze kumiliki mapenzi na wanawake nao wanatafuta vipato vikubwa na kubadilisha maisha yao kupitia mchezo huo unaolipa. Vijana kwa pamoja wanakuwa Wamepotea katika lindi la kutafuta mali na kujipatia hadhi ya kimapenzi

Hapo napo kuna maisha ya wasanii ambao hufanya kazi ili zipendwe wajiingizie kipato. LAKINI kazi hizo hupitia kwenye Media kuwafikia mashabiki

Katika kupotea huko kwa vijana na Jamii yote hapo hapo kuna faida na ahueni kwa Watawala na Wanasiasa. Watawala wanazo pesa lakini hapo hapo wanahita uungwaji mkono wa kisiasa. Watu hawazingatii undani wa masuala, wanazingatia pesa na ili pesa zao ziwe na nguvu lazima Watu wazamie katika starehe na uasherati huku wao wakiwa wanajijengea familia imara. Rushwa na hongo hata kama ni ndogo inapata kipaumbele cha hali ya juu na hiyo huwahakikishia uungwaji mkono katika Siasa zao na kujikita madhubuti katika Utawala

Media huwachagulia watu maudhui ya kuwafikia, Mtawala / Mwanasiasa kupitia Media na wasanii ndio wanaochuja na kuchagua wasanii wapi wawe na Umaarufu na wawe na mafanikio kuwashinda wale ambao ni kinyume na maslahi yao. Kama msanii anachokipaji na amekubali matakwa yao basi atachuma ya juu kutoka kwa Watawala / Wanasiasa na Media pia kutoka kwa Mashabiki.

Muziki wetu wa Bongo fleva na Bongo Hip hop umebadilika sana na sasa haujengi chochote. Mziki wa Singeli ndio kabisaaa ujinga mtupu. Lawama ziende kwa Wanasiasa na Watawala wetu ambao wamezishika media na wasanii.

Mwanamke akikubali kuolewa amekuba kutoa mapenzi bure – Jamaa anarudi na robo kilo ya nyama, unga na vitu vingine vidogo vidogo na anataka mapenzi bila kupimiwa. Hapo ndio utakapo uona ufa utokanao na siasa zetu.

Wasanii wa miaka ya 90 na mwanzo wa 2000 ndio hao hawapewi nafasi au lazima wabadilike. Tumpe mauwa B2K Mnyama, Ali Kiba na wengineo ambao wamekataa kuyumba.

CCM ni tatizo na Ndoa inageuka kuwa ni upuuzi mwingine katika jamii hii. Mara wasanii wanaambiwa “Toeni nyimbo zenye maadili ya kufundisha jamii” mara “Wasanii badilisheni maudhui” – Hayo ni mashairi katika wimbo wa Joh Makini uitwao “Content”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *