Familia ndio msingi wa Taifa, Ndani ya familia ndipo ambapo malezi sahihi na makuzi wa watoto na vijana hupatikana kwa usahihi. Ni wajibu kwa jamii kushirikiana kwa pamoja kuilinda taasisi ya familia
Msingi mzuri wa familia ni ndoa, Ndoa ambayo ni muungano wa watu wawili, mke na mume walioamua kuishi pamoja na kuunda familia. Familia zikiwa imara mambo ya kijamii yanakuwa yanakwenda bila mushkeli. Familia nzuri hutupatia watu ambao wanafaa kuaminiwa katika nafasi mbali mbali na watu ambao ni hakikisho la jamii na kizazi kizuri katika muendelezo wake.
Lazima ziwepo sheria mahsusi kabisa za kupambana na mitikisiko inayoikumba taasisi ya familia, Uislamu unazosheria kali sana ambazo huilinda taasisi ya familia na kuwalazimisha wana jamii wote kuitegemea taasisi hiyo kwa ajili ya kupata mapenzi au kuwa na watoto
Lengo la chapisho hili sio kuuwawa kwa wazinifu bali ulinzi dhidi ya wale wafanyao vitendo ambavyo huleta mapinduzi, mfarakani au kutowesha amani katika taasisi ya ndoa na familia. Kama sheria zinaruhusu wengine kuishi maisha bila ya ndoa basi uwepo mstari wa wazi wa kuwatenganisha na wale wanaotegemea ndoa kama nguzo muhimu katika maisha yao ya kifamilia
Kuna kesi nyingi sana za talaka na mauji kwa sababu ambayo inatolewa kirahisi tu kama “Wivu wa mapenzi”. Ipo haja ya Jamii yetu kuwa na sheria madhubuti za kuwalinda wahanga ambao wanaweza kuchukua hatua mbaya kama mauwaji na kujitia matatizoni kwa kupata kesi mbaya ikiwemo ya mauwaji
Iwepo sharia ya “Uhaini ngazi ya familia” ili kudhibiti vitendo vya kupanga njama na kuharibu familia au ndoa halali za watu wengine. Sheria iweke wazi faini na kifungo cha yoyote atakaye shiriki katika njama hizo awe ni mwanafamilia au mtu wa nnje. Kuna msemo usemao wa “Wa nje husaidiwa na wa ndani” kwa hiyo hadi familia inapata madhara basi wapo wa ndani hasa baba na mama ambao ndio nguzo ya familia ambao kwa namna moja au nyingine wamehusika.
Sheria ifafanue wazi adhabu ya makosa kama ugoni (Kufumaniwa), kuzaa na mke wa mtu, kuzaa na mme wa mtu, mme kupuuza majukumu yake, mke kupuuza majukumu yake
Makosa ya kuzaa kando na ugoni ni matokea ya njama bila kujali athari ya matendo hayo kwa wenza wao, Mtu wanje anakula njama na mtu wa ndani na kuleta mtafaruku na sintofahamu ndani ya familia husika, huo nao ni uhaini katika ngazi ya familia
Watu hupatwa na Sonona, Uchizi, homa, uzubaifu, kokosa hamu ya kula, huzuni na kushindwa kufanya kazi. Kuwapa fidia watu hao na kuwaadhibu wakosaji kutatoa faraja kubwa sana na kuepushia mbali matatizo ya watu kujichukulia sharia mikononi na kusababisha uharibifu wa mali na kudhuriana
Sheria hiyo pia iangazie baadhi ya mambo yanayotokea katika uchumba na kuwalinda wale ambao watakuwa ni wahanga wa vitendo vya kishenzi ambavyo havizingatii ustaarabu na mila zetu

