Watu wabaya wanatengenezwa. Kuna mazingira yanawafanya watu wawe na tabia za dhambi na za kihalifu na kuna mazingira yanawafanya watu wewe watenda wema na wazuri kwao wenyewe, familia zao na jamii yote kwa ujumla.
Maisha magumu na kukwama katika umaskini kunafanya wawe tayari kufanya kazi yoyote na kuna baadhi ya watu wanafikia hatua ya kufanya kazi za hatari na za kihalifu. Wanajikuta wameishiwa machaguo na kufanya kazi ambazo zitaathiri mustakabali wao na familia zao.
Viongozi kushiriki njama na magendo pia kunapelekea jamii kuwa na watu ambao huona kufanya kazi za halali hazileti maendeleo haraka na kuupindua ukweli wa watu kuona kuwa kufanya kazi za halali ni hatari na hazifanikiwi kama zile za magendo na kushiriki njama na fitina.
Watu wazuri kufeli maisha, kuishi kwa huzuni na upweke, Hii hupelekea watu kuwa njia panda, Baraka kwa watu wema ziko wapi? Kuna faida gani ya kuishi maisha matakatifu? Watu wanaona ni bora waishi mbali na maisha masafi ya kiimani ili wapate furaha na mafanikio katika maish yao
Kukithiri kwa uonevu, unyanyasaji na ubaguzi kwenye jamiii hupelekea watu kuona ya kuwa kuishi maisha ya kutenda wema ni udhaifu na mamna ya kujiweka hatarini kwa kuonewa, kudhulumiwa na inafika hatua wanaona ni bora na wao wawe waoevu, wanyanyasaji na wabaguzi
Wapo watu ambao wanafanya maovu na dhambi kwa sababu walidharauliwa na hisia zao hazikuheshimiwa. Wakaamini kuwa wao ni duni na hawana thamani kwa watu wanaowapenda au watu ambao hugusa maisha yao moja kwa moja
Kuhadaana na kutumiana kimapenzi pia kuna weza kupelekea wahanga kuona thamani yao imechezewa na kosa lao ni kupenda kwa moyo na kujitoa kwa ajili ya kudumisha penzi. Wapo wanawake wanakuwa Malaya kwa sababu wanaona mapenzi ni kudanganyana. Wapo wanaume hugeuka Malaya baada ya kuona hawapendwi na thamani yao iko kwenye pesa zao
Zumbe10D na Dunia Isiyo na dhambi
Mifumo yangu ya Kiuchumi, Kimapenzi na kiimani inaweza kupukutisha dhambi duniani na zikabaki kwa udogo sana na zikakosa mashiko
Mfumo wangu wa kutowesha Umaskini na kuwa na Usawa na utajiri duniani na kuanzisha dunia mpya isiyotumia fedha, Isiyo na biashara, isiyo na bank wala mikopo. Dunia ya kila kitu bure. Hakuna cha kuiba, Hakuna kununua mapenzi, Hakuna cha kufisadi, hakuna cha kudhulumu, hakuna cha kutapeli na hakuna cha kulangua. Ni dunia ambayo hakuna kuwaza kuhusu kesho labda miaka 10 ijayo au Zaidi.
Masuala ya kiuchumi yanaathiri masuala ya kimapenzi na familia. Nyumba umepewa buru, Chakula bure, Nguo bure, fanicha za ndani bure na vitu vingine vya chumbani, sebleni na jikoni; Vyote bure. Dunia itakuwa ya Mapenzi ya kweli haswa, Uwezo wako wa kupenda, kubembeleza, kuimba, kujaza matumaini, kutunza ahadi, kujali na kuzingatia na kujitolea ndio vitakupatia Mpenzi – Mume / Mke na kudumu naye.
Kulala peke yako bila kipenzi ni hiari yako au hukufuata kanuni za mapenzi kwa hiyo utajilaumu mwenyewe.
Ndoa za mapema zitapewa umuhimu mkubwa na mapenzi ya Jinsia tofauti yatatawala. Hakuna wanaume wawili watalala pamoja tangia balehe, hili litatatuliwa kwa mimi Ahmad Ten’dii niliyetukuka kupewa Utawala wa Dunia na kuifanya Bustani
Kuhusu Imani inayoweza kuwaunganisha watu wa duniani basi ni Imani ya Zumbe10d, Watu watafuata Imani zao kwa uhuru na matendo ya siyo ya “Karama” yatakataliwa wazi wazi ikibidi yatapewa hadhi ya Jinai. Pamoja kwenye haki Yangu mimi Ahmad Ten’dii niliyetukuka ni kukua tu, hakuna kudumaa, kukua tu hadi mawinguni. Roho safi zitapewa Nafasi ya juu sana na kupalilia na kuenziwa hadi watu wenye wa Roho chafu wajihisi wamechelewa na walichezea sana muda kwenye maisha yao
Ufalme wa Haki na uanzishaji wa Taifa lisilo na mipaka, Kisha tunajenga taifa na taifa linatutuza. Taifa litasimama kwa Haki yangu mimi mwenyewe Ahmad, mkweli, muaminifu, mwenye akili nyingi, Mtunza ahadi na Aliyekosa ubinafsi.
Unakaribishwa wote katika Unyenyekevu na Utiifu na uadhimishaji wa Ahmad Ten’dii aliyetukuka
Tafadhali toa maoni yako chini ukurasa huu

