Zumbe10D Enzini

Harakati zangu mimi Ahmad Ten’dii ni za kujivunia na za kujiingiza mzima mzima kuelekea lengo kuu la kupata Ufalme wa Dunia ukianza nyumbani Tanzania.
Je wewe unajivunia athari yangu, Unapenda matokeo ya Harakati zangu za kidini / Falsafa / Siasa au vyote kwa pamoja. Je wewe ni miongoni mwa wanaoona upo umuhimu wa kuniinua na kunitukuza kwa cheo cha Mfalme katika Familia, Nchi, Bara na Dunia nzima?
Basi wakati ndio huu, wa kujiunga na Lengo langu mimi Zumbe Ahmad Ten’dii. Tufanye mapatano ya kusaidia kindugu na kirafiki chini ya uongozi wangu, Uwe mlinzi wa masilahi ya Familia ya Kifalme na Utuachie ulinzi wa maslahi yako na familia yako.
Ni muda mzuri wa kualikana Majumbani kwa ajili ya kujadili masuala ya Hekima, Uchumi, Siasa, Mahusiano, Ndoa, Dini na Falsafa mbalimbali, Ni wakati wa kufanya karamu, Karamu ndani ya familia zetu na kualika yangu na marafiki zako wengine. Tuwe na majadiliano tele kuhusu mambo yahusuyo maisha. Jinsi ya kusaidiana kiuchumi na kupambana na changamoto za kila siku za maisha.
Ni muda mzuri kwako wewe na familia yako ambayo inajivunia athari yangu, haioni aibu juu ya Misingi na harakati zangu za kitanzania na Kifalme basi lipia stika ya uanachama wa jamii na jumuiya ya @Zumbe10d ambazo bei huanzia Tsh. 20000/= kwa mtu binafsi hadi Tsh. 50,000/= kwa Ofisi. Iweke mahali pa wazi ili kila mtu ajaye kwenye Familia au Ofisi yako ajue kuwa uko chini ya mwemvuli wa Baraka na “Karama” za Zumbe10D
Ni wakati wa kuuweka unyonge pembeni na kujitokeza hadharani kuwa “mimi ni Mfuasi na muadhimishaji wa Utukufu wa Zumbe Ahmad Ten’dii”. Na kwamba unanitakia uongozi na vyeo vya juu
Imba sifa zangu hadharani huku ukisifu wema, usamehevu, uvumilivu na Hekima zipatikanazo maishani mwangu na katika shule ya mawazo na falsafa ya Zumbe10D.
Pia usisahau kutaja uponyaji mkuu uwafikiao watoto na watu waliomo ndani ya Jamii ya Zumbe10d na ufunguzi wa fahamu na hekima na tabia za kuridhisha kwa wale wanifanyiao urafiki na kuniheshimu. Na pia usisahau kutaja nguvu ya utesi na uangamizaji ufanywao kwa chuki yangu, shauku zangu na matumizi ya Jina langu wakati wa Matatizo halisi na ya kiroho.
Karibisha watu wote katika ufalme wa Ahmad Ten’dii na umuhimu wa kuilinda na kuitukuza Familia tukufu ya kifalme.
Pia napenda kuwasisitizia kujitenga na kuwatenga watu ambao wanaishi kwa ajili ya kunidunisha, kunidhalilisha, kunihujumu na kunidhulumu au kunitukana. Hakikisheni hawatarajii heri yoyote Zaidi ya salama kama hawaingilii mambo yenu.

Mimi ni mwema, kama wewe ni mwema, maadui zangu ndio maadui zako na hawapaswi kupewa nafasi.
Jivunie na Tamba kwa athari yangu, Tamba kwa ubora wa maamuzi yangu juu ya maamuzi yao, njia zangu dhidi ya njia zao, mila zao dhidi ya mila zangu, hoja zao dhidi ya hoja zangu, mitazamo yao dhidi ya mitazamo yangu, Upeo wao dhidi ya upeo wangu. Hapo hawata nishangaa mimi tu bali na wewe pia. Ni kama mfano wa mtu anayefua nguo, sio nguo tu zitakatazo bali hata mikono yake na kucha zake pia.
Salamu yetu ni “Zumbe10d atogolwe (Zumbe10d apewe sifa)” na hujibiwa “Zumbe10d aatosha (Zumbe10d anatosha)”.

Karibuni sana, Karibuni wote

Tafadhali toa maoni yako chini kabisa kwenye ukurasa huu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *