Ni Wakati Wa Kumtambua Mfalme.

Ni kweli kabisa, Kuna watu unapowazungumzia huwezi ukawatenga na Dini zao. Na mimi ni Mmoja wao. Lakini Hatuna Budi kutambua na Kuheshimu kuwa tunaishi kwenye Dunia yenye Dini Mseto. Mimi na Heshimu hilo na nimewasisitiza Wanangu na Wafuasi wangu kuheshimu hilo.

Huwezi Ukatumia Dini yangu kunikwamisha Kisiasa au Kiuchumi, Hiyo ni Dhuluma ya wazi ukizingatia kuwa Dini yangu ni miongoni mwa Dini Nzuri ambazo huunga mkono Ustawi wa Wanadamu na Mazingira yake kwa hali ya Juu kabisa

Lakini pia Sijasahau nafasi ya Serekali ya Tanzania na Mipaka yake na Sera zake katika Kutumika na kuingizwa kwa Falsafa na Mawazo yangu katika Jamii Yetu

Lakini pia Natambua Demokrasia tulionayo inaweza kutumika kuidhinisha Mwanzo wa Familia Yangu kuwa Nguzo katika Nguzo za Utawala wa Nchi hii na kuwa Familia Rasmi kwa ajili ya kuhifadhi mila nzuri na Utamaduni wa Mtanzania, Mwafrika na Mkazi wa Dunia kuanzia Milenia hii na kuendelea

Nimeshafundisha na kuandika Misingi mingi sana ya Ustaarabu na nimeshapambana na Ushenzi wa Sampuli nyingi sana. Kwa hiyo basi ni Wakati wa kuinua Utajo wangu na wa Familia niikuzayo kwa ajili ya kulinda na kuhifadhi ustaarabu na Ustawi wa Taifa na Dunia Yetu kwa ujumla

Waingereza Wanao msemo usemao kuwa “Charity begins at home” wakimaanisha Sadaka huanzia Nyumbani. Kwa hiyo Heshima ya Familia ya Kifalme inapaswa itambuliwe na Serekali ya Tanzania Kwanza kabla ya Jamii yoyote ya Mbali na Hapa maana matokeo yake hayatavutia sana

Tunaweza kuanza kuwa waalikwa kwenye Sherehe na Matukio ya Serekali na Baadae kukwea hadhi ya kuwa Viongozi kwenye Sherehe na Matukio ya Nchi. Naamini kabisa thamani ya Maoni yangu Pendwa na wengi ambayo yametumika kuboresha Maisha, maamuzi na hukumu za wengi yanapata hadhi yake endapo yataambatana na Mashauri ya Kiserekali.

Tunakuwa hatuonekani tena kama Wapinzani bali Washirika wa Serekali. Mambo yatabadilika, Itakuwa tu sio jambo la fahari kuiga Mtindo wangu wa Maisha na Muingiliano na Watu bali litakuwa rahisi na Jambo linalowezekana kwa msaada wa kijamii pale inapohitajika

Ndio, Dini yangu ndio inayoweza kuwaunganisha Watanzania na Walimwengu maana Mgogoro uliopo juu ya Mungu yupi na wa namna gani afuatwe haupo kwetu, Kwetu ni “Karama” tu. Tunauheshimu Uislam, Ukristo, Ubuda na dini nyingine kwa kuwaandaa watu kuishi kwa “Karama” na Wakija kwetu (Familia ya Zumbe10d) hawatabaguliwa wala kudhuluwa chochote hata kama ni kidogo.

Tafadhali toa maoni yako chini kabisa kwenye ukurasa huu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *